Historia ya Hifadhi Bahari

 

Historia ya Maeneo Tengefu ya Bahari nchini Tanzania ilianza katikati ya miaka ya 1970 ambapo maeneo nane (8) yalichapishwa katika gazeti la serikali kama hifadhi za bahari chini ya Sheria ya Uvuvi Na.6 ya Mwaka 1970. Hadi mwaka 1994 ndipo Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) kilipoanzishwa kwa Sheria Namba 29.
MPRU ni Taasisi ya Serikali inayojitegemea na yenye jukumu la kuanzisha, kuendeleza na kusimamia Hifadhi za Bahari na Maeneo yake Tengefu Tanzania. MPRU inafanya kazi chini ya Bodi ya Wadhamini ambayo inasimamia utekelezaji wa shughuli zake. Bodi ya Wadhamini iko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Tangu kuanzishwa kwa MPRU, mipango na taratibu mbalimbali zimeanzishwa ili kuhakikisha uendelevu wa rasilimali za pwani na bahari, utunzaji wa makazi-bahari, uboreshaji wa ustawi wa viwango vya maisha ya jamii na mchango wao wa kiuchumi kwa ujumla katika maendeleo ya nchi.