MAFUNZO YA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA SAMIKI KIDIGITALI
MAFUNZO YA UKUSANYAJI WA TAKWIMU ZA SAMIKI KIDIGITALI

Mafunzo ya ukusanyaji takwimu kwa njia ya kidigitali katika mfumo wa eCAS yakiedelea. Mafunzo haya ni  ya muda wa siku 10 kuanzia tarehe 16/10/2023 hadi 26/10/2023, jumla ya washiriki 12 ambao ni wakusanya takwimu 6 kutoka katika vijiji vya Chemchem, Mibulani, Kiegeani, Bwejuu na Jibondo pia wafanyakazi 6 kutoka katika Hifadhi ya Bahari ya Mafia. Mafunzo haya yanatolewa na wakufunzi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Taasisi ya Utafiti (TAFIRI) pamoja na IT kutoka MPRU.